Dua ya safari.

1

( 207 ) “Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa; ametakasika ambaye ametudhalilishia sisi hiki (chombo au huyu mnyama), na hatukuwa sisi kwacho ni wenye uwezo, na sisi kwa Mola wetu tutarejeshwa. Ewe Mwenyezi Mungu hakika sisi tunakuomba katika safari yetu hii wema na ucha Mungu, na katika matendo unayoyaridhia, Ewe Mwenyezi Mungu ifanye nyepesi safari yetu hii, na ufupishe umbali wake, Ewe Mwenyezi Mungu, Wewe ndie Mwenzangu katika safari, na Mchungaji wa familia yangu, Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi najilinda kwako kutokana na ugumu wa safari, na ubaya wa mtizamo, na uovu wa kubadilikiwa katika mali na familia.” Wakati wa kurudi safari atayasema haya yalioko juu na kisha atazidisha: “Tunarudi, hali ya kuwa tunatubia, tunaabudu, na Mola wetu tunamsifu.”

Zaker copied