( 196 ) “Kutakasika ni kwako Ewe Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni zako, nakiri kwamba hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, nakuomba msamaha na ninarejea kwako.” Imepokewa kutoka kwa Aisha (R.A) amesema: ‘Hajapatapo kukaa Mtume (ص ) kikao, wala kusoma Qur’ani, wala kuswali ila atamaliza na dua hii.’ Amesema Aisha (R.A) nikamuuliza,' ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nakuona hukai kikao chochote wala husomi Qur'ani wala huswali swala yoyote ile ila unaimalizia kwa kusoma maneno haya, kwanini hasa? Akasema; Ndio anaisema kheri amalize kwa kheri, na anaesema shari yanakuwa maneno haya nikafara kwake. “Kutakasika ni kwako, na sifa njema zote ni zako, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, nakuomba msamaha, na ninarejea kwako.”