( 160 ) “Ewe Mwenyezi Mungu mlinde na adhabu ya kaburi.” “Ewe Mwenyezi Mungu mjaalie kuwa nikitangulizi na akiba kwa wazazi wake na nikiombezi chenye kukubaliwa dua yake. Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yake zifanye nzito mizani za wazazi wake na yafanye mengi malipo yao, namkutanishe na wema wa waumini, na mjaalie awe katika dhamana ya Ibrahim na umuepushe kwa rehema yako na adhabu ya moto, na mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake, na jamaa bora kuliko jamaa zake, Ewe Mwenyezi Mungu wasamehe waliotangulia, na waliopita, na waliotutangulia katika Uislamu.” Alikuwa Al-Hassan (رضي الله عنه ) anamsomea mtoto mdogo Suratul-Fatiha kisha akisema:
( 161 ) “Ewe Mwenyezi Mungu. mfanye kwetu sisi ni kitangulizi cha malipo, na dhamana, namalipo.”