Dua ya kumuombea maiti wakati anaposwaliwa.

1

( 156 ) “Ewe Mwenyezi Mungu msamehe na umrehemu, na umuafu, na msamehe, na mtukuze kushuka kwake (kaburini), na upanue kuingia kwake, na muoshe na maji, na kwa theluji, na barafu, na mtakase namakosa, kama unavyo takasa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake, na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na muingize peponi na mkinge na adhabu ya kaburi [na adhabu ya moto].”

2

( 157 ) “Ewe mwenyezi Mungu msamehe aliyehai katika sisi na aliye kufa, na aliyopo na asiyekuwepo, na mdogo kati yetu na mkubwa, na mwanamume kati yetu na mwanamke. Ewe Mwenyezi Mungu unaemueka hai kati yetu basi mweke katika uislamu, na uliyemfisha basi mfishe juu ya imani. Ewe Mwenyezi mweke katika uislam, na unayemfisha usitupoteze baada yake.”

3

( 158 ) “Ewe Mwenyezi Mungu hakika fulani bin fulani yuko katika dhima yako, na kamba ya ujirani wako basi mkinge na fitina ya kaburi na adhabu ya moto nawe ndiwe mstahiki wa utekelezaji na ukweli, basi msamehe na umrehemu hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu.’’

4

( 159 ) “Ewe Mwenyezi Mungu, mja wako na mtoto wa kijakazi chako, nimuhitaji wa rehema yako, nawe huhitaji na kumuadhibu, kwa hivyo akiwa ni mwema mzidishie katika mema yake, na akiwa ni muovu msamehe madhambi yake.”

Zaker copied