Dua anayoomba mgonjwa aliyekata tamaa na kupona.

1

( 150 ) “Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe mimi, na uni rehemu, na unikutanishe na waja walio katika daraja za juu.”

2

(151) Imepokewa kutoka kwa Aisha (R.A) amesema: ‘Mtume ( ص) wakati anakufa alikuwa akiingiza mikono yake ndani ya maji kisha akipangusa kwayo uso wake na akisema; “Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki, ila ni Mwenyezi Mungu ,hakika kifo kina uchungu.”

3

( 152 ) “Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu peke yake, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, mpeke hana mshirika wake, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, ni wake Ufalme, na sifa njema zote ni zake, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, na hapana uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.”

Zaker copied