Amesema Mtume ( ص ): 'Mumini mwenye nguvu ni bora na anapendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko mumini dhaifu, na wote wana kheri, fanya pupa kwa kile kitakacho kunufaisha na taka msaada kwa Mwenyezi Mungu wala usichoke, na kikikupata kitu chochote kibaya basi usiseme lau kama ningefanya kadha na kadha yasingenitokea haya, lakini sema: ( 144 ) Amepanga Mwenyezi Mungu na analolitaka anafanya. ” .....hakika neno Ia lau linafungua matendo ya shetani. Hakika Mwenyezi Mungu analaumu mwenye kukata tamaa, lakini usivunjike moyo, na ukishindwa na jambo kabisa sema: “Mwenyezi Mungu ananitosheleza, naye ni Mbora wa kutegemewa.”