Dua ya mwenye kuogopa dhulma ya mwenye kutawala.

1

( 129 ) Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa mbingu saba, na Mola wa arshi tukufu, kuwa mlinzi wangu kutokana na fulani bin fulani, na vikosi vyake miongoni mwa viumbe vyako, kwakunisaliti mmoja miongoni mwao, au kunifanyia uadui, amehishimiwa mwenye umelinda, nazimetukuka sifa zako, na hapana mola apasae kuabudiwa kwa uhaki, ila Wewe.’’

2

(130) Mwenyezi Mungu ni mkubwa, Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu(cheo) kuliko viumbe vyake vyote, Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu, kuliko kila nikiogopacho nakujihadhari, najikinga na Mwenyezi Mungu, ambae hapana mola ila yeye tuu, ambae ameshikililia mbingu saba, ili zisi angukie ardhi, ila kwa idhini yake, kutokana na shari ya mja wako fulani, na majeshi yake, nawanae mfuata, na wafuasi wake, miongoni mwa majini na watu. Ewe Mwenyezi Mungu, kuwa mlinzi wangu kutokana nashari yao, zimetukuka sifa zako, na umehishimika ulinzi wako, nalime takasika jina lako, na hapana apasae kuabudiwa kwa uhaki, asie kuwa Wewe.

Zaker copied