( 120 ) “Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ni mtumwa wako, mtoto wa mtumwa wako, mtoto wa kijakazi chako, utosi wangu uko mikononi mwako, yaliyopita kwangu yako katika hukumu yako, ni usawa kwangu kunihukumu kwako, nakuomba kwa kila jina ambalo ni Lako ulilojiita kwalo Mwenyewe, au uliloliteremsha katika kitabu chako, au ulilomfundisha yoyote yule kati ya viumbe vyako, au ulilolihifadhi Wewe mwenyewe (na kujihusisha kulijuwa) katika ilimu ilio fichika kwako, nakuomba uijaalie(uifanye) Qur’ani, kuwa ni raha na uchanuzi wa roho yangu, na nuru ya kifua changu, nautatuzi wa huzuni yangu, nasababu ya kuondoka majonzi yangu.”
( 121 ) “Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na hamu na huzuni na kutoweza na uvivu na ubakhili na uoga na uzito wa deni na kushindwa na watu.”