Dua ya Qunut ya Witri

1

( 116 ) ”Ewe Mwenyezi Mungu, niongoze pamoja na uliowaongoza, na unipe afya njema, pamoja nauliowapa afya njema, na nifanye kuwa nimpenzi wako, pamoja na ulio wafanya wapenzi, na nibariki katika ulichonipa, na nikinge na shari ya ulilolihukumu, kwani Wewe unahukumu wala huhukumiwi, hakika hadhaliliki uliemfanya mpenzi [wala hatukuki uliemfanya adui] Umetakasika Ewe Mola wetu na Umetukuka.”

2

( 117 ) “Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na kwa msamaha wako kutokana na adhabu yako, na najilinda kwako kutokana na Wewe, mimi siwezi kuzidhibiti sifa zako, Wewe ni kama ulivyojisifu Mwenyewe.”

3

( 118 ) “Ewe Mwenyezi Mungu, Wewe tu ndie tunaabudu, na kwako tunasali na tunasujudu, na kwako tunakimbilia na tunakutumikia, tunataraji rehema yako, na tunaogopa adhabu yako, kwani adhabu yako hakuna shaka kuwa makafiri itawafikia. Ewe Mwenyezi Mungu hakika sisi tunakutaka msaada, na tunakutaka msamaha, na tunakusifu kwa kheri, na wala hatuku kufurishi, na tunakuamini Wewe, na tunakunyenyekea na tunamuepuka anaekukufuru.”

Zaker copied