Anayoyafanya mwenye kuota ndoto njema au mbaya.

1

Ndoto njema inatoka kwa Mwenyezi Mungu na ndoto mbaya inatoka kwa mashetani. (114) Akiona mmoja wenu ndoto nzuri asimzungumzie ila yule anaempenda, na anaeona ndoto mbaya anatakiwa apulize kushotoni kwake mara tatu. -Kisha atake (aombe) hifadhi, kwa Mwenyezi Mungu na alichokiona, na kwa shetani mara tatu. - Kisha hatakiwi kumzungumzia mtu. - Kisha asilalie ule upande au ubavu aliyootea, bali ageuke ubavu mwengine.

Zaker copied