Nyiradi za kulala.

1

(99) Alikuwa Mtume (ص ) akienda kulala usiku anakusanya viganja vyake kisha akivipuliza na akivisomea Suratul-Ikhlas, na Suratul—FaIaq, na Suratu—Nnas, kisha akipangusa kwa hivyo viganja vyake kiasi anachoweza kalika mwili wake, akianza kichwani na usoni na mbele. (Akifanya hivyo mara (am).

2

(100) Mtume (ص ) amesema: 'Ukienda kulala soma Ayatul-Kursiy mpaka uimalize kwani Mwenyezi Mungu ataendelea kukuhifadhi, wala hakukaribii shetani mpaka asubuhi. ' { اللّهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لاَ تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلاَ نَوْمٌ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلاَّ بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلاَ يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلاَّ بِمَا شَاء وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ وَلاَ يَؤُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ } [ Suratul-Baqarah:255 ]

3

(101) Amesema Mtume (ص ) : ‘Anaesoma aya mbili za mwisho wa Suratul-Baqarah usiku zinamtosheleza. ' {آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللّهِ وَمَلآئِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لاَ نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ وَقَالُواْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ * لاَ يُكَلِّفُ اللّهُ نَفْساً إِلاَّ وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ رَبَّنَا لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا وَلاَ تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْراً كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا رَبَّنَا وَلاَ تُحَمِّلْنَا مَا لاَ طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا أَنتَ مَوْلاَنَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ} mpaka mwisho wa sura). (Suratul| - Baqarah: 285-286)

4

(102) Mtume ( ص ) pia amesema: 'Akiamka mmoja wenu kutoka usingizini kasha akarudi basi akikukute kitanda kwa shuka yake mara tatu, na amtaje Mwenyezi Mungu, kwani hajui kilicho kuja baada yake. Na akilala aseme: “Kwa jina lako Mola wangu, nimeweka ubavu wangu na kwa ajili yako nitaunyanyua, na ukiizuia (ukiichukuwa) roho yangu, basi irehemu, na ukiirudisha basi ihifadhi, kwa kile unacho wahifadhi nacho waja wako wema.”

5

( 103 ) “Ewe Mwenyezi Mungu hakika Wewe umeiumba nafsi yangu nawe utaiua, ni kwako uhai wa nafsi yangu na ufaji wake, ukiipa uhai basi ihifadhi, na ukiifisha (ukiiua) basi isamehe. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba afya njema.” Alikuwa Mtume ( ص ) akitaka kulala, anaweka mkono wake wa kulia chini ya shavu lake, kisha anasema:

6

( 104 ) Ewe Mwenyezi Mungu nikinge mimi kwa adhabu yako siku utakayo wafufua waja wako. (Mara tatu)

7

( 105 ) “Kwa jina lako Ewe Mwenyezi Mungu ninakufa na ninakuwa hai.”

8

( 107 ) “Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa mbingu saba, na Mola wa arshi tukufu, Mola wetu, na Mola wakila kitu, Mwenye kuichanua tembe ya mbegu na kokwa, na alie teremsha Taurat na Injiil,na Qur’ani, najikinga kwako, kutokana na shari ya kila kitu, Wewe ndie mwenye kukamata utosi wake, Ewe Mwenyezi Mungu, wewe ndie wa Mwanzo, hakuna kabla yako kitu, nawe ndie wa Mwisho, hakuna baada yako kitu, nawewe ndie uliewazi, hakuna juu yako kitu chochote, na Wewe ndie uliefichika, hakuna kilicho jificha chini yako, tulipie madeni yetu, na utuepushe na ufakiri.”

9

( 106 ) Mtume ( ص ) amesema: ‘Hivi niwafahamishe juu ya kitu ambacho ni bora zaidi kuliko mtumishi, wakati munapolala; msabihini Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu, kisha msifuni Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu, na kisha mkabirini mara thelathini na nne, kwani kufanya hivi ni bora kwenu kuliko mtumishi. ’ (Yaani useme: “Ametakasika Mwenyezi Mungu” ( mara thelathini na tatu ) “Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu.” ( mara thelathini na tatu ) “Mwenyezi Mungu ni mkubwa.” ( mara thelathini na nne )

10

( 108 ) Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye ametulisha na ametunywesha na akatutosheleza na akatuhifadhi, ni wangapi ambao hawana wa kuwatosheleza wala wa kuwahifadhi.”

11

( 109 ) “Ewe Mwenyezi Mungu Mjuzi wa yaliojificha na yaliowazi , Muumba wa mbingu na ardhi, Mola wa kila kitu na Mfalme wake, nakiri kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, najilinda kwako na shari ya nafsi yangu na shari ya shetani na shirki yake, na kujichumia uovu kwa nafsi yangu au kumletea muislamu.”

12

(110) Mtume ( ص ) alikuwa halali mpaka asome Suratu-Sajda na Suratul-Mulk. Ukiraka kulala tawadha udhu kama wa swala kisha lalia ubavu wako wa kulia kisha useme:

13

( 111 ) “Ewe Mwenyezi Mungu nimeisalimisha nafsi yangu kwako, na nimekuachia mambo yangu Wewe, na nime uelekeza uso wangu kwako, na nimeutegemeza mgongo wangu kwako, kwa matarajio na kwa kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa ila kwako, nimekiamini kitabu chako ulicho kiteremsha, na mtume wako uliyemtuma.” Amesema Mtume ( ص ) kwa mwenye kusema haya: ‘Kisha ukifa utakuwa umekufa katika uislamu. '

Zaker copied