( 75 ) قرآن [Suratul-Baqa.rah:255] Mwenye kuisoma (Ayatul-Kursiy) pindi anapoamka atalindwa kutokana na majini mpaka jioni, na atakaeisoma jioni atalindwa nayo mpaka asubuhi.
( 76 ) قرآن na قرآن (Mara tatu tatu) Mwenye kuzisoma (sura hizi) mara tatu asubuhi na jioni zinamtosheleza na kila kitu.
(77 ) “Tumeingia wakati wa asubuhi na umekuwa Ufalme ni wa Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni za Mwenyezi “Mungu, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki, ila Mwenyezi Mungu, hali yakuwa peke yake, hana mshirika, niwake Ufalme, nanizake sifa njema, nayeye juu yakila kitu ni Mueza, Ewe mola; nakuomba kheri ya siku ya leo, na kheri ya baada ya siku hii, nanina jilinda kwako, kutokana na shari ya siku ya leo, na shari ya baada ya siku hii, Ewe Mola, najilinda kwako, kutokana na uvivu, na ubaya wa uzee ( uzee ubaya), Ewe Mola; najilinda kwako, kutokana na adhabu ya moto, na adhabu ya kaburi.” Na akiingia jioni, atasema:
( 78 ) “Ewe Mwenyezi Mungu kwa sababu yako tumeingia katika asubuhi, na kwa ajili yako tumeingia jioni, na kwa ajili yako ndio tumekuwa hai, na kwa ajili yako tutakufa, na kwako tutafufuliwa.” Na ikifika jioni atasema: “Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako tumefika jioni, na kwa ajili yako tumefika asubuhi, na kwa ajili yako tukohai, na kwa ajili yako tutakufa, na nikwako tuu marejeo.”
( 79 ) “Ewe Mwenyezi Mungu Wewe ni Mola wangu, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, umeniumba mimi, na mimi ni mja wako, nami niko juu ya ahadi yako, na agano lako, kiasi cha iwezo wangu, najilinda kwako, kutokana na shari ya nilicho kifanya, nakiri kwako kwa kunineemesha, nanakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unisamehe kwani hasamehe madhambi ila Wewe.” kwa haki ila Wewe, umeniumba mimi, na mimi ni mja wako, nami nikojuu ya ahadi yako, na kiaga chako, kiasi cha uwezo wangu, najilinda kwako kutokana na shari ya nilichokifanya, narejea kwako kwa kunineemesha, na narejea kwa madhambi yangu, basi nakuomba unisamehe, kwani hasamehe madhambi ila Wewe.”
( 80 ) “Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nimefika asubuhi nakushuhudia na nina washuhudiza wabeba wa arshi yako, na malaika wako, na viumbe vyako vyote, kwamba Wcwe ndiye Mwenyezi Mungu, hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, hali ya kuwa peke yako huna mshirika, na kwamba Muhammad ni mja wako, na ni mtume wako.” (Atasema hivi mara inne, asubuhi au jioni). ...atakae yasema haya asubuhi au jioni mara inne, Mwenyezi Mungu (S.W) atamuepusha na moto.
( 81 ) “Ewe Mwenyezi Mungu sikuamka na neema yoyote au kati ya kiumbe chako chochote, na neema ila inatoka kwako, hali ya kuwa pekeyako huna mshirika wako, ni zako sifa njema na nizako shukrani.” ....atakae yasema haya kila asubuhi basi atakuwa ametekeleza shukrani ya siku nzima, na atakae yasema jioni atakuwa ametekeleza shukrani ya usiku mzima.
( 82 ) “Ewe Mwenyezi Mungu nipe afya ya mwili wangu, Ewe Mwenyezi Mungu nipe afya ya usikizi wangu, Ewe Mwenyezi Mungu nipe afya ya uwoni wangu, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe”. (mara tatu) “Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na ukafiri, na ufakiri, na najilinda kwako kutokana na adhabu ya kaburi, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe.” (mara tatu)
( 83 ) “Mwenyezi Mungu ananitosha, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Yeye, kwake Yeye nimetegemea, na Yeye ni Mola wa arshi tukufu.” (mara saba asubuhi na jioni)
( 84 ) “Ewe Mwenyczi Mungu nakuomba msamaha na afya duniani na akhera. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba msamaha na afya katika dini yangu, na dunia yangu najamaa zangu, na mali yangu, Ewe Mwenyezi Mungu nisitiri uchi wangu, na unitulize khofu yangu, Ewe Mwenyezi Mungu ni hifadhi mbele yangu, na nyuma yangu,na kulia kwangu, na kushoto kwangu, najuu yangu, na najilinda kwa utukufu wako kwakutekwa chini yangu.”
( 85 ) “Ewe Mwenyezi Mungu, Mjuzi wa yaliyojificha na yaliyowazi, Muumba wa mbingu na ardhi, Mola wa kila kitu, na Mfalme wake, nakiri kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, najilinda kwako kutokana na shari ya nafsi yangu, na shari ya shetani na shirki yake, na kujichumia uovu kwa nafsi yangu au kumletea muislamu.”
(86 ) Kwa jina la Mwenyezi Mungu, ambae hakidhuru kwa jina lake kitu chochote kile kilicho ardhini, wala mbinguni, nae ni Msikivu nani Mjuzi.” (mam tatu).
( 87 ) “Nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndie Mola wangu, na uislamu ndio dini yangu, na Muhammad ( ص ) kuwa ni Mtume wangu.” (mara tatu)
( 88 ) “Ewe Uliyehai, Uliyesimama kwa dhati yako, kwa rehema zako ninakuomba uniokoe, nitengenezee mambo yangu yote, wala usiniachie mambo yangu mwenyewe (pasina kunisaidia), hata kwa muda (mdogo kama muda) wa kupepesa jicho.”
( 89 ) “Tumeingia asubuhi, na imefika asubuhi na Ufalme ni wa Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe vyote, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba kheri ya siku hii ya leo, ufunguzi wake, na nusra yake, na nuru yake, na baraka yake, na uongofu wake, na najilinda kwako kutokana na shari ya kilicho ndani ya siku hii, na shari ya baada ya siku hii.” Na ikiingiajioni atasema:
( 90 ) “Tumeingia asubuhi na maumbile ya kiislamu, na neno la ikhlasi, na dini ya Mtume wetu Muhammad ( ص ) na mila (dini) ya baba yetu Ibrahim iliyo sawa hali yakuwa muislamu wala hakuwa ni mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu.” Na ikiingiajioni atasema:
( 91 ) “Ametakasika Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote nizake.” (mara mia moja)
( 92 ) “Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, peke yake, hana mshirika wake, niwake Ufalme, na nizake sifa njema zote, na Yeye juu ya kila kitu ni Mueza.” (mara kumi, au mara moja ukisikia uvivu) Amesema Mtume ( ص ) : ‘Mwenye kusema inapoingia asubuhi:
( 93 ) “Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu peke yake, hana mshirika wake, niwake Ufalme, na nizake sifa njema zote, na Yeye juu ya kila kitu ni Mueza.” .... ..kwa siku mara mia, basi yeye ana thawabu za kuwaacha huru watumwa kumi na ataandikiwa thawabu mia moja, na atafutiwa madhambi mia moja, na atakuwa na kinga ya shetani kwa siku hiyo yore hadi jioni, na hata kuwa mtu yoyote mbora kumshinda, iIa yule aliyefanya zaidi yake.
( 94 ) Ametakasika Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni zake, kwa hisabu ya viumbe vyake, na radhi yake, na uzito wa arshi yake, na wino wa maneno yake.” ( mara tatu kila asubuhi)
( 95 ) “Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba elimu yenye kunufaisha, na riziki iliyo nzuri, na ibada yenye kukubaliwa.”
( 96 ) “Namuomba msamaha Mwenyezi Mungu, na ninarejea Kwake.” (Mara mia kwa siku) Alikuwa Mtume (ص ) akisema asubuhi na jioni:
( 98 ) “Ewe Mwenyezi Mungu mfikishie rehema na amani Mtume wetu Muhammad.” 'Mwenye kuniombea rehema asubuhi mara kumi, na jioni mara kumi, nitamuombea shifaa (msamaha) siku ya kiama. ’