Dua ya Swalatul-Istikhara (swala ya kutaka muelekezo au kukata shauri katika jambo).

1

(74) Amesema Jaabir bin Abdillah ( رضي الله عنه ): ‘Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ( ص ) akitufundisha Swala ya Istikhara kama vile anavyotufunza sura ya Qur'an, anasema ( ص ): ‘Akikusudia mmoja wenu kufanya jambo aswali rakaa mbili zisizo za faradhi, kisha aseme: “Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakutaka muelekezo kwa ujuzi wako, na nakuomba uniwezeshe kwa uwezo wako, na nakuomba fadhila zako kubwa, hakika Wewe unaweza, nami siwezi nawe unajua nami sijui, nawe nimjuzi wa yale yalio fichikana. Ewe Mwenyezi Mungu, iwapo jambo hili kutokana na ujuzi wako - (atalitaja jambo lake) - linakheri na mimi katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu (karibu au mbali) basi nakuomba uniwezeshe ni lipate, na unifanyie wepesi, kasha unibariki, na iwapo unajua kwamba jambo hili ni shari kwangu katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu ( karibu au mbali) basi liepushe na mimi nami niepushe nalo, na nipangie jambo jengine lenye kheri nami popote lilipo, kisha niridhishe kwalo.” Na hajuti mwenye kumtaka muelekeo Mwenyezi Mungu, na akawashauri waja waumini, na akajidhatiti katika jambo lake. Amesema Mwenyezi Mungu (SW) kumwambia Mfume wake ( ص ) قرآن “Na ushauriane nao katika mambo, na ukiazimia kufanya jambo, basi tegemea kwa Mwenyezi Mungu.” ( Suratu Al- Imran: 159)

Zaker copied