Nyiradi baada ya kutoa Salamu (kumaliza Swala).

1

( 66 ) “Namuomba msamaha Mwenyezi Mungu.” (mara tatu) “Ewe Mwenyezi Mungu Wewe ndie Amani, na kwako ndiko kutokako amani, Umetukuka Ewe mwenye utukufu, na Ukarimu.”

2

( 67 ) “Hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake hana mshirika, niwake Ufalme, na nizake sifa njema, na yeye ni muweza wa kila kitu, Ewe Mwenyezi Mungu, hapana anaeweza kukizuia ulichokitoa, na wala kutoa ulichokizuia, na wala haumnufaishi mwenye utajiri, kwani kwako Wewe ndio utajiri.”

3

( 68 ) “Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake hana mshirika wake, ni wake Ufalme, na nizake sifa njema, na Yeye juu ya kila kitu ni Mueza, hapana uwezo wala nguvu ila vyote vinatokana na Mwenyezi Mungu, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, wala hatumuabudu ila Yeye, nizake neema, na niwake ubora, na nizake sifa nzuri zote, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, hali ya kumtakasia dini yake, ijapokuwa wanachukia makafiri”

4

( 69 ) “Ametakasika Mwenyezi Mungu (mara thelathini na tatu ) Sifa njema zote niza Mwenyezi Mungu” (mara thelathini na tatu ) “Mwenyezi Mungu ni Mkubwa” ( mara thelathini na tatu ) “Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa peke yake hana mshirika wake, ni wake Ufalme, na ni zake sifa njema, na Yeye ni Mueza wa kila kitu.” Kisha atasoma: Suratul-Ikhlas, na Suratul—Falaq na Suratu—Nnas, yaani -

5

( 70 ) Kisha atasoma: Suratul-Ikhlas, na Suratul—Falaq na Suratu—Nnas, yaani - kila baada ya swala mara moja. na baada ya swala ya Magharibi na ya Alfajiri atazisoma hizo mara tatu tatu. Pia ni katika Sunnah kusoma Aayatul- Kursiy baada ya kila swala. Nayo ni:

6

{ اللّهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لاَ تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلاَ نَوْمٌ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلاَّ بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلاَ يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلاَّ بِمَا شَاء وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ وَلاَ يَؤُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ }

7

( 72 ) “Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki, ila Mwenyezi Mungu, hali yakuwa peke yake, hana mshirika wake, ni wake Ufalme, na nizake sifa njema, anahayaisha, anafisha, na yeye nimuweza kwa kila kitll.” (Mara kumi baada ya Swala ya Alfajiri na ya Magharibi)

8

( 73 ) “Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba elimu yenye kunufaisha, na riziki iliyo nzuri, na ibada yenye kukubaliwa.” (Baada ya kutoa Salamu ya Swala ya Alfajiri).

Zaker copied