Dua baada ya Tashahhud.

1

( 55 ) Ewe Mwenyezi Mungu mimi nakutaka unihifadhi na adhabu ya kaburi, na adhabu ya (moto wa) jahannam, na fitna ya uhai, na ya kufa, na shari ya fitna ya Masihi-ddajjal”

2

( 56 ) Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na najilinda kwako kutokana na fitna ya Masihi-dajal, na najilinda kwako kutokana na fitna ya uhai na ya mauti, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na dhambi na deni.”

3

( 57 ) “Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi nime idhulumu nafsi yangu, dhulma kubwa, na hasamehe madhambi ila Wewe, basi nisamehe msamaha kutoka kwako, na unirehemu, hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu.”

4

( 58 ) Ewe Mwenyezi Mungu ni samehe niliyo ya tanguliza, na niliyo ya chelewesha, na niliyo ya fanya kisiri na niliyo ya fanya kwa dhahiri, na niliyo ruka mipaka, na ambayo Wewe unayajua zaidi kuliko mimi, Wewe ndiwe mwenye kutanguliza, na Wewe ndiwe mwenye kuchelewesha, hakuna apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe.”

5

( 59 ) Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie kukukumbuka, na kukushukuru, na uzuri wa kukuabudu.”

6

( 60 ) Ewe Mwenyezi Mungu najilinda kwako kutokana na ubakhili, na najilinda kwako kutokana na uwoga, na najilinda kwako kutokana na kurudishwa kwenye umri duni, na najilinda kwako kutokana na fitna ya dunia na adhabu ya kaburi.”

7

( 61 ) Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba pepo, na najilinda kwako kutokana na moto.”

8

( 62 ) “Ewe Mwenyezi Mungu, kwa ujuzi wako wa mambo yalio fichikana, na uwezo wako wa kuumba, niweke hai iwapo uhai ni bora kwangu, na nifishe iwapo kufa ni bora kwangu, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba khofu yako kwa siri na dhahiri, na ninakuomba neno la haki wakati nimefurahi na wakati nimekasirika, na ninakuomba matmnizi ya wastani wakati wa utajiri na wakati wa umaskini, na ninakuomba neema isiyokwisha, na ninakuomba kituliza jicho (moyo) kisicho katika, na ninakuomba kuridhia baada yakuwa umesha nipangia, na nina kuomba maisha ya utulivu, baada ya kufa, na nina kuomba ladha yakukutizama uso wako, na shauku yakukutana nawe, pasina madhara yanayodhuru, wala fitna yenye kupoteza, Ewe Mwenyezi Mungu, tupambe kwa kipambo cha imani, na tujaalie tuwe waongozi wenye kuongoka.”

9

( 63 ) “Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba, Ewe Mwenyezi Mungu kwa vile Wewe ni Mmoja ulie pekee, Mwenye kutegemewa kwa haja zote, ambae hakuzaa wala hakuzaliwa, na wala hakuna mfano wake na kitu chochote, nakuomba unisamehe makosa yangu, hakika Wewe ni Mwingi wa kusamche, Mwenye kurehemu.”

10

(64 ) “Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi nakuomba, kwa vilesifa njema zote ni zako, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, hali yakuwa pekeyako, huna mshirika, mwingi wa kuneemesha, Ewe mtangulizi (muumbaji) wa mbingu na ardhi, (bila kuwa na mfano kabla), Ewe mwenye utukufu na ukarimu, Ewe alie hai mwenye kusimama kwa dhati yako,hakika mimi nakuomba Pepo, na najilinda kwako kutokana na moto.”

11

( 65 ) “Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba kwa vile ninakiri kwa hakika kwamba Wewe ni Mwenyezi Mungu, hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, hali ya kuwa pekee, mwenye kutegemewa kwa haja zote, ambae hakuzaa wala hakuzaliwa, na wala hakuna mfano wake na kitu chochote.”

Zaker copied