Kumsalia Mtume ( ص ) baada ya tashahhud.

1

( 53 ) Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Muhammad na jamaa zake Muhammad, kama ulivyo mrehemu Ibrahim, na jamaa zake Ibrahim, hakika Wewe ni Mwenye kusifika Mtukufu, Ewe Mwenyezi Mungu mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad, kama ulivyo mbariki Ibrahim na jamaa zake Ibrahim, hakika Wewe ni Mwenye kusifika Mtukufu.”

2

( 54 ) Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Muhammad, na wake zake, na kizazi chake, kama ulivyo warehemu jamaa wa Ibrahim. Na mbariki Muhammad, na wake zake, na kizazi chake, kama ulivyo wabariki jamaa zake Ibrahim, hakika Wewe Umesifika na Umetukuka.”

Zaker copied