( 31 ) Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, sifa njema niza mwenyezi mungu, kwa wingi na sifa njema ni za mwenyezi mungu, kwa wingi, na sifa njema ni za mwenyezi Mungu kwa wingi, na ametakasika Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni.” (Atasema haya mara tatu). Najilinda na Mwenyezi Mungu kutokana na shetani, na kupulizia kwake, na kutabana kwake na kutia kwake wasiwasi katika nyoyo za binadamu.” Mtume ( ص ) alikuwa akiamka usiku, ili kufanya ibada anasema:
( 27 ) Ewe Mwenyezi Mungu niweke mbali na madhambi yangu kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi, Ewe Mwenyezi Mungu nitakase na madhambi yangu kama vile inavyo takaswa nguo nyeupe na uchafu, Ewe Mwenyezi Mungu nisafishe na madhambi yangu kwa theluji na kwa maji na kwa barafu.”
( 28 ) “Kutakasika ni kwako, ewe Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni zako, na limetukuka jina lako, na utukufu niwako, na hapana apasae kuabudiwa kwa haki, asie kuwa Wewe.
( 29 ) Nimeuelekeza uso wangu kwa yule ambae ameumba mbingu na ardhi hali ya kumtakasia yeye dini yangu, na sikuwa mimi ni katika washirikina, hakika swala yangu na kuchinja kwangu na uhai wangu, na kufa kwangu ni kwa Mwenyezi Mungu Bwana wa viumbe vyote, hana mshirika, na kwa hilo nime amrishwa, nami ni katika waislamu, Ewe munyezi mungu, wewe ndie mfalme, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila wewe, wewe ndie bwana wangu na mimi ni mtumwa (mja) wako, nimeidhulumu nafsi yangu, na nimekiri madhambi yangu kwa hivyo nisamahe madhambi yangu yote, hakika hasamehe madhambi, ila Wewe. Na niongoze kwenye tabia njema (nzuri), kwani haongoze kwenye tabia nzuri, ila Wewe, niepushe na tabia mbaya, kwani hakuna mwenye uwezo wakuniepusha na tabia mbaya, ila Wewe, naitikia mwito wako, naninafuraha kukutumikia, na kheri zote ziko mikononi mwako, na shari haitoki kwako, mimi nimepatikana kwa ajili yako, na nitarudi kwako, umetakasika, na umetukuka, nakutaka msamaha naninarejea kwako (kwa kutubia) .
( 30 ) Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa Jibriil na Miikaail na Israafil, Muumba wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa mambo yaliojificha na yaliowazi, Wewe unahukumu baina ya waja wako katika mambo ambayo walikuwa wakitafautiana, niongoze mimi kwenye haki katika yale waliotafautiana kwa ruhusa yako, hakika Wewe unamuongoza umtakae kwenye njia ilionyoka.”
( 32 ) Ewe Mwenyezi Mungu nizako sifa njema, Wewe ndie nuru ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake; na nizako sifa njema, Wewe ndie sababu ya kusimama kwa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake; na nizako sifa njema, Wewe ndiwe Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake; na nizako sifa njema, ni wako Ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake; na nizako sifa njema, Wewe ndiwe Mfalme wa mbingu na ardhi, na nizako sifa njema, Wewe ni Haki (kweli), na ahadi yako ni yakweli, na neno lako ni lakweli, na kukutana na Wewe ni kweli, na pepo ni kweli, na moto ni kweli, na Mitume ni kweli, na Muhammad ( ص ) ni kweli, na Qiyama ni kweli, Ewe Mwenyezi Mungu, kwako nime jisalimisha, na kwako nime tegemea, nawewe nime kuamini, na kwako nimeregea, na kwa ajili yako nimeteta, na kwako nimehukumu, kwa hivyo nisamehe niliyo yatanguliza, na niliyo yachelewesha, na niliyo yaficha na niliyo yatangaza; Wewe ndie mwenye kutanguliza na Wewe ndie mwenye kuchelewesha, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe; Wewe ndie Mola wangu, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe.