Dua za Adhan.

1

Mtu akisikia Muadhini anaadhini anatakiwa aseme kama anavyo sema Muadhini, ila atakapo sema: ( 22 ) ‘Hayya ala swalaah’ “Njooni kwenye swala.” ‘Hayya alal falaah’. “Njooni kwenye mafanikio.” yeye hato muigiza, bali anatakiwa aseme: ‘Laa Haula walaa quwwata illaa billah.’ “Hapana uwezo wala nguvu ila za Mwenyezi Mungu.” Muadhini akisema; Ash-hadu anla ilaha illa Laah, ash-hadu anna Muhammada Rrasuulu Laah, Anatakiwa mtu aseme:

2

( 23 ) Na mimi pia nakiri kwa moyo, na kusema kwa ulimi,kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki, ila mwenyezi mungu Mmuja peke yake, hana mushrika wake, na kwamba Muhammad ni mja wake, na ni mtume wake,nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndie bwana wangu, na kuwa Muhammad ni Mtume wangu, na kuwa Uislamu ndio dini yangu.”

3

( 25 ) “Ewe Mwenyczi Mungu, bwana wa mlingano(mwito) huu uliotimia, na sala ilio simama, mpe (Mtume) Muhammad Wasila, na fadhila, na mfikishe daraja yenye kusifiwa, ambayo umemuahidi, (kwani wewe hukhalifu ahadi)” .

4

(26) Inafaa kwa mtu kujiombea kati ya Adhana na Iqamah, kwani dua kati ya Adhana na Iqamah hairudishwi.

5

(24) Kisha baada ya kumjibu Muadhini atamswalia Mtume ( ص ) . Kisha atasema:

Zaker copied