Katika mambo ya kheri na adabu kwa jumla.

1

(267) ‘Ikiingia jioni (yaani jua linapokuchwa wakati wa magharibi) wazuieni watoto wenu kutoka toka kwani mashetani wanatawanyika nyakati hizo, ikisha pita wakati waacheni. Na fungeni milango na mtajeni Mwenyezi Mungu mnapoifunga, kwani shetani hafungui mlango ulio fungwa. Na fungeni viriba vyenu vya maji, na mtajeni Mwenyezi Mungu. Na finikeni vyombo vyenu, na mtajeni Mwenyezi Mungu, (finikeni) hata kama ni kwa kuwekea kitu juu. Na zimeni taa zenu. ' Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu na mbariki Mtume wetu Muhammad (ص), maswahaba wake, familia yake, na wote wanaowafuata katika uongofu mpaka siku ya malipo. Amiin.

Zaker copied