Fadhila za Tasbiih, na Tahmiid, na Tahliil, na Takbiir.

1

(254) Amesema Mtume (ص): ‘Mwenye kusema: “Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema zote ni zake”. Kwa siku mara mia, atafiuiwa madhambi yake hata kama yalikuwa mfano wa povu la bahari. '

2

(255) Na Mtume (ص) amesema: ‘Atakaye sema: “Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake, hana mskirika, ni wake Ufalme, na ni zake kila sifa njema, na Yeye juu ya kila kitu ni Mueza”. .... ..mara kumi, ni kama (thawabu za mtu) aliyewacha huru nafsi nne katika wamz wa Ismail.’

3

(256) Na amesema Mtume (ص): 'Kuna maneno mawili ni mepesi mno juu ya ulimi, mazito mno katika mizani, yanapendeza mno mbele ya Rahmani (Mwenye kurehemu) nayo ni: “Ametakasika Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni zake, ametakasika Mwenyezi Mungu aliye Mtukufu.”

4

(257) Na amesema Mtume (ص): ‘Kusema Kwangu: “Ametakasika Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa”. ..... ..ni bora kwangu kuliko kila kilichoangaziwa na jua. ’

5

(258) Na amesema Mtume (ص): ‘Hivi anashindwa mmoja wenu kuchuma kila siku thawabu elfu ?' Mtu mmoja miongoni mwa waliokaa akamuuliza; ‘Atachuma vipi mmoja wetu thawabu elfu ?’ Akamjibu (ص) ‘Aseme: “Ametakasika Mwenyezi Mungu” ..mara mia moja, basi ataandikiwa thawabu elfu moja, au atafutiwa madhambi elfu moja.

6

(259) Na Mtume (ص) amesema: ‘Atakaesema: “Ametakasika Mwenyezi Mungu aliye Mtukufu, na sifa njema zote ni zake.” …..hupandiwa mtende peponi.

7

(260) Na amesema Mtume (ص) : “Ewe Abdallah bin Qais, hivi nikufahamishe (nikuonyeshe) hazina miongoni mwa hazina za pepo? Nikamwambia: Ndio Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akaniambia, “Sema: “Hakuna uwezo wala nguvu ila za Mwenyezi Mungu.”

8

(261) Na akasema (ص): ‘Bora ya maneno kwa Mwenyezi Mungu ni manne: “Ametakasika Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa.” .....sivibaya kuanza kwa lolote katika haya.'

9

(262) Alikuja mtu mmoja wa shamba kwa Mtume (ص) akamwambia, nifundishe maneno nitakayo yasema, Mtume (ص) akamwambia: ‘Sema: “Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake, wala hana mshirika wake, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa tena sana, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu tena nyingi sana, Ametakasika Mwenyezi mungu ni Mkubwa, tena vyote, hapana uwezo wala nguvu ila ni za Mwenyezi Mungu, Mwenye Kutukuka, Mwingi wa Hekima.” .... ..yule mtu kisha akasema, ‘Haya ni ya Mwenyezi Mungu, ni yapi yangu ?’ Mtume (ص) akamwambia, ‘Sema: “Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe, na unirehemu, na uniongoze, na uniruzuku.”

10

(263) Alikuwa mtu akisilimu, Mtume (ص) anamfundisha kuswali kasha anamuamrisha kuomba kwa matamshi haya: “Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe, na unirehemu, na uniongoze, na unipe afya njema, na uniruzuku.”

11

(264) ‘Bora ya dua ni mtu kusema: “Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.” na bora ya utajo(uradi) ni mtu kusema: “Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu.”

12

(265) ‘Mema yasiokwisha ni : “Ametakasika Mwenyezi Mungu, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, na hakuna uwezo wala nguvu ila za Mwenyezi Mungu.”

Zaker copied