Kuomba msamaha na kutubia.

1

(248) Amesema Mtume (ص): ‘Na apa kwa Mwenyezi Mungu hakika mimi ninamtaka msamaha Mwenyezi Mungu na ninatubia kwake katika kila siku zaidi ya mara sabini.’

2

(249) Mtume (ص ) pia amesema: ‘Enyi watu tubieni kwa Mwenyezi Mungu kwani mimi ninatubia kwake kwa siku mara mia.

3

(250) Pia Mtume (ص ) amesema: “yoyote anaesema: “Namuomba msamaha Mwenyezi Mungu, Mtukufu, ambaye hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Yeye, aliye Hai, aliyesimama kwa dhati yake, na ninarejea kwake.” ..... ..Mwenyezi Mungu atamsamehe hatakama ana makosa ya kukimbia vitani.’

4

(251) Amesema mtume ( ص) “Wakati anaokuwa mja na Mola wake, wako karibu zaidi, nikatika nusu ya mwisho ya usiku. Ukiweza kuwa miongoni mwa wanaomtaja Mwenyezi Mungu, kwa wakati huo, basi kuwa.

5

(252) Mtume (ص ) pia amesema: ‘Sehemu ambayo anakuwa mja yuko karibu mno na Mala wake ni wakati amesujudu, basi zidisheni dua wakati huo. '

6

(253) Mtume (ص ) amesema: ‘Huwa nimesahaulishwa kumtaja Mwenyezi Mungu, na hakika mimi ninamuomba msamaha Mwenyezi Mungu mara mia kwa siku. ’

Zaker copied