Dua ya kusomwa ukiwa umesimama katika mlima wa Swafaa na wa Maruah.

1

Amesema Jaabir ( رضي الله عنه ): ‘Mtume ( ص ) alipokurubia Swafaa alisoma: ( 236 ) “Hakika Swafaa na Marwah ni katika alama za kumtukuza Mwenyezi Mungu.” “Ninaanza kwa alichoanza Mwenyezi Mungu.” …… akaanza Swafaa akapanda mpaka Akaiona Al-Kaaba kisha akaielekea, na kusema: “Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa.” .... .. kisha atasema yafuatayo mara tatu akiomba dua (yoyote ile apendayo) baada ya kila mara: “Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake, wala hana mshirika wake, ni wake Ufalme, na ni zake sifa njema, naye juu ya kila kitu ni Mueza. Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake, ametekeleza ahadi yake, na amemnusuru mja wake, na amevishinda vikosi peke yake.” ....M!ume ( ص ) alisoma hivi mara tatu na baina yake akiomba dua, kisha akafanya akiwa Marwah kama alivyofanya Swafaa.

Zaker copied