Fadhila za kueneza na kudhihirisha maamkuzi ya Kiislamu.

1

(224) Amesema Mtume ( ص ): ‘Hamtaingia peponi mpaka muamini, na hamtakuwa waumini wa kweli mpaka mpendane. Hivi Niwafahamishe kitu mkikifanya mtapendana? Salimianeni baina yenu.’

2

(225) Amesema Ammar bin Yaasir ( رضي الله عنه ): ‘Mambo matatu anaeyakusanya basi amekusanya Imani; uadilifiz wa nafsi yako, na kutowa salamu kwa watu wote, na kutoa (sadaka) hali ya kuwa ni mchache wa mali. ’

3

(226) Imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Omar (رضي الله عنه ) kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume ( ص ) ‘Ni uislamu gani bora ?’ Mrume ( ص ) akamjibu, 'KuIisha (maskini) na kumsalimia unaemjua na usiemjua.'

Zaker copied