Fadhila za kumswalia Mtume ( ص)

1

(219) Amesema Mtume ( ص ): ‘Yoyote atakaeniswalia mimi mara moja, basi Mwenyezi Mungu atamswalia mara kumi.'

2

(220) Na amesema Mtume ( ص ) Musilifanye kaburi langu kuwa ni Idi, (mahali pa kufanywa ibada inayo rejewa rejewa), na niswalieni kwani kuniswalia kwenu kunanifikia popote mulipo. ’

3

(221) Pia amesema Mtume ( ص ) : ‘‘Bakhili ni yule ambaye nikitajwa haniswalii.

4

(222) Na amesema Mtume( ص ) : “Hakika Mwenyezi Mungu, ana malaika wanazunguka katika ardhi, wananiletea salamu kutoka kwa ummah wangu.

5

(223) Na pia akasema Mtume( ص ): Hakuna mtu yoyote anaenisalia, ila Mwenyezi Mungu hunirudishia roho yangu, ili nimurushie salamu.

Zaker copied