Anachosema mtu iliyemjia habari ya kufurahisha au ya kusikitisha.
﷽
1
(218) Alikuwa Mtume ( ص ) ikimjia habari ya kufurahisha akisema:
“Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye kwa neema yake yanatimia mambo mema.”
Na ikimjia habari ya kusikitisha husema:
“Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu kwa hali zote.”