Dua ya msafiri akirudi kutoka safarini.

1

(217) Imepokewa kutoka kwa Ibn Omar (R.A) kwamba Mtume ( ص ) alikuwa akirudi vitani au kutoka Hijjah katika kila akipanda mlima akisema: “Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa.” kisha akisema: “Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki, ila mwenyezi mungu, hali ya kuwa peke yake, wala hana mshirika ufalme ni wake, na sifa njema ni zake, na Yeye juu ya kila kitu ni Mueza, tunarudi hali ya kuwa tunatubia, tunaabudu, na Mola wetu tunamsifu, amesadikisha Mwenyezi Mungu ahadi yake, na amemnusuru mja wake, na amevishinda vikosi peke yake.”

Zaker copied