Dua za kuamka kutoka usingizini.

1

( 1 ) “Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambae ametupa uhui baada ya kutufisha na ni kwake tu kufufuliwa.” Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ( ص ): ‘Mwenye Kushutuka usingizini usiku akasema:

2

( 2 ) “Hapana mola, apasae kuabudiwa kwa haki ila mwenyezi mungu, hali yakuwa peke yake hana mshirika, ni wake ufalme, na ni zake sifa njema, na yeye juu ya kila kitu ni muweza, ametakasika mwenyezi mungu, na sifa njema zote ni zake, na hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni mwenyezi mungu, na Mwenyezi Mungu ni mkubwa, na hapana uwezo wala nguvu, isipokuwa vyote vinatokana na Mwenyezi Mungu, alie juu, alie mtukufu, ewe Mola(Mwenyezi Mungu); nisamehe.” ..basi atasamehewa. Na kama atasimama akaenda kutawadha, akaswali, basi swala yake atakubaliwa.

3

( 3 ) Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambae amenipa uzima wa mwili wangu, na akanirudishia roho yangu, na akaniruhusu kumtaja.”

4

quran

Zaker copied